Mchezaji wa zamani
wa Timu ya taifa ya Brazil Carlos Dunga ametimuliwa kwenye nafasi ya
Kocha wa Brazil kufuatia Nchi hiyo kutupwa nje ya Michuano ya Copa
America na Peru.
Shirikisho la Soka la Brazil, CBF, limetoa
taarifa ya kumtimua Dunga ambaye pia alitarajiwa kuiongoza Nchi hiyo
kwenye Michezo ya Olimpiki ambayo itachezwa nchini Brazil mwezi Agosti.Pamoja na Dunga, pia Wasaidizi wake wote wa Benchi la Ufundi wameondolewa, na CBF imesema itateua Watu wengine kuingoza Timu hiyo.
Brazil ilifungwa 1-0 na Peru, Goli linaloelezwa kuwa la mkono, na kutupwa nje ikiwa ni mara yao ya pili tu katika Historia ya Miaka 100 ya Mashindano hayo kushindwa kuvuka hatua ya Makundi.
Dunga, ambae alikuwa nahodha wa Brazil Mwaka 1994 walipobeba Kombe la Dunia, aliteuliwa kuwa Kocha wa Brazil mara baada ya Nchi hiyo kutolewa kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 zilizochezwa kwao Brazil.
Lakini tangu atwae wadhifa huo, ikiwa ni mara yake ya pili kuwa Kocha wa Brazil, Nchi hiyo haijafanya vyema na kutolewa Nusu Fainali ya Copa America ya 2015 kwa Penati na Paraguay ambayo ilifanyika nchini Chile
ConversionConversion EmoticonEmoticon