Rais wa Simba Evans Aveva, alisema kuwa usajili wa Ibrahimu utasaidia kuimarisha timu hiyo ambayo ina kiu ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu ujao.
“Ni kweli tumempa mkataba wa miaka miwili jana mchana (juzi), na bado tunaendelea kufanya mazungumzo na wachezaji wengine, lengo letu ni kujenga timu yetu na pia kuhakikisha msimu ujao tunafanya vizuri,” alisema Aveva.
Kauli ya Aveva imekuja huku wanachama wa klabu hiyo ya Msimbazi wakiwa na kiu ya kutwaa ubingwa na kushiriki michuano ya kimataifa ambayo kwa mwaka wa nne mfululizo wameikosa.
Huyo ni mchezaji wa pili kutoka Mtibwa kusajiliwa na Simba, ambapo wa kwanza alikuwa kiungo Muzamir Yassi. Simba pia tayari imeibomoa Mwadui kwa kuwasajili wachezaji wake Emmanuel Semwanza na Jamal Mnyate.
“Tulikuwa hatutaki kuona masuala yetu ya usajili yanafanyika kwa uwazi, kwa sababu nusu ya wachezaji tunaowahitaji kwa ajili ya kuwasajili wana mikataba na timu zao, hivyo inabidi tumalizane kwanza na klabu zao ndio tunaweka wazi, ” alisema Aveva.
Alipotafutwa Meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo kuzungumzia hilo, alikiri taarifa hizo kuwa za kweli mchezaji huyo maarufu kwa jina la Rasta kusaini mkataba wa miaka miwili Simba.
“Rasta amesaini mkataba jana (juzi) na hapa ninapoongea na wewe, ndiyo tunamalizana kwa maana ya kusaini mkataba huo wa miaka miwili,” alisema Kisongo
ConversionConversion EmoticonEmoticon